Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda

BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA ZANZIBAR

Malengo na Majukumu

LENGO LA KUANZISHWA ZNBC

Lengo kuu la kuanzishwa Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar ni pamoja na:

  • Kuandaa mikutano ya majadiliano baina ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwa dhamira ya kupata muafaka na uwelewa juu ya mambo ya msingi yanayohusiana na usimamizi na ukuaji wa uchumi.
  • Kuzidisha ukuaji wa uchumi ili kupunguza umaskini na kuendeleza maendeleo endelevu.
  • Kutathmini maendeleo ya mazingira ya kibiashara ya ndani na nje, changamoto, na fursa ili kupata suluhisho.
  • Kubadilishana uzoefu juu ya mazingira yaliyopo ya uendeshaji na usimamizi wa biashara kwa lengo la kuboresha utendaji mzuri wa biashara na utoaji wa huduma.
  • Kutathmini na kupendekeza uimarishaji wa kimazingira ya Kibiashara yatakayowavutia wawekezaji na ushindani wa kibiashara.
  • Kuzingatia jambo jengine lolote ambalo litapelekea kwa Baraza la Taifa la Biashara kufikia malengo yake.

MAJUKUMU YA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA LA ZANZIBAR

    Kwa Mujibu wa Kifungu namba 9 cha Sheria ya kuundwa kwa Baraza la Taifa la Biashara la Zanzibar Baraza lina majukumu yafuatayo:

    • Kukuza mashirikiano ya sekta ya umma na sekta binafsi.
    • Kuweka utaratibu wa majadiliano ya kibiashara baina ya sekta ya umma na sekta binafsi.
    • Kuyapitia mambo yanayoanzia katika mikutano au majadilianao ya Jukwaa yanayohusiana na maendeleo ya kiuchumi na kushauri njia sahihi za utatuaji kwa utekelezaji kwa sekta husika.
    • Kufanya au kupelekea kufanywa utafiti juu ya sera za maendeleo ya kijamii na kiuchumi kama Baraza litakavyoona inafaa.
    • Kupitia utekelezaji wa maazimio ya Baraza kwa sekta inayohusika.
    • Kupokea kupitia na kutoa mapendekezo juu ya sera, tafiti, taarifa au mapendekezo yaliyowasilishwa kwenye Baraza na Sekta husika yanayohusiana na biashara na maendeleo ya kiuchumi.
    • Kuweka malengo pamoja na muda wa utekelezaji wake kwa utekelezaji wa miongozo, maamuzi au maazimio ya Baraza.
    • Kusimamia na kutathmini utekelezaji wa kazi za Baraza.