Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda

BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Mwinyi ameongoza Mkutano wa jukwaa la Kumi na mbili la Biashara Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa (SMIDA) Bw. Soud Said Ali, akitembelea maonesho ya Wafanyabiashara katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 19-3-2023, wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Kumi na Mbili la Biashara Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Jijini Zanzibar,(kushoto kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrissa Mustafa Kitwana.