Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda

BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA ZANZIBAR

Muundo

MUUNDO WA SASA NA MGAWANYO WA MAJUKUMU (KIIDARA, KIDIVISHENI NA KIVITENGO).

Baraza linaongozwa na Sekretarieti ya Baraza la Taifa la Biashara ambayo ipo chini ya Katibu Mtendaji na inawajibika kwa Mheshimiwa Waziri anaeshughulikia masuala ya Biashara. Muundo pia umezingatia majukumu ya msingi na uwezo wa ZNBC kwa mujibu wa sheria Nam 10 ya mwaka 2017 na majukumu yake ya msingi ambayo ni kukukuza mashirikiano ya baina Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. 

Muundo wa sasa wa Baraza una Idara mbili na Vitengo vitano (5) ambavyo vipo chini ya Katibu Mtendaji. Ufafanuzi wa majukumu ya Idara/Ofisi ya Uratibu Pemba na Vitengo ni kama ifuatavyo:-

  1. Idara ya Mipango na Uratibu wa Majadiliano
    • Divisheni ya Mipango na Utafiti.
    • Divisheni ya Uratibu Majadiliano.
    • Divisheni ya Ufuatiliaji.
  2. Idara ya Utawala na Fedha. 
    • Divisheni ya Utawala na Uendeshaji.
    • Divisheni ya Uhasibu.

A. Idara ya Mipango na utaratibu wa Majadiliano

Idara hii ina jukumu la kuendesha majadiliano ya kibiashara baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika kuweka mazingira mazuri ya biashara na kujenga uelewa na kuaminiana.  Idara hii itakuwa na kitengo cha Mipango na Utafiti, kitengo cha Uratibu wa majadiliano na kitengo cha Ufuatiliaji.

Majukumu ya Idara ya Mipango na Uratibu wa Majadiliano:

  • Kuandaa mikutano ya majadiliano baina ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi  ii. Kutathimini maendeleo ya mazingira ya kibiashara ya ndani na nje, changamoto, na fursa ili kupata suluhisho.
  • Kubadilishana uzoefu juu ya mazingira yaliyopo ya uendeshaji na usimamizi wa biashara kwa lengo la kuboresha utendaji mzuri wa biashara na utoaji wa huduma.
  • Kutathmini na kupendekeza uimarishaji wa kimazingira ya Kibiashara yatakayowavutia wawekezaji na ushindani wa kibiashara. na
  • Kuandaa vipeperushi vinavyoeleza miongozo na taratibu zinazoongoza mfumo wa endeshaji wa Majadiliano.
  • Kufanya utafiti na tathmini ya mfumo wa uendeshaji wa majadiliano kila baada ya muda ili kuangalia kama mfumo huo unaendana na mazingira mazuri ya ufanyaji biashara na ukuaji wa uchumi.
  • Kuandaa mapendekezo ya bajeti ya ZNBC. viii. Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ZNBC.  ix. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mpango mkakati, mpango kazi na mpango wa matumizi wa Baraza (cash flow).
  • Kukusanya taarifa za uchambuzi wa takwimu zinazohitajika katika kutayarisha mipango pamoja na mapendekezo ya bajeti.
  • Kuandaa miradi ya maendeleo ya ZBC na kutafuta wafadhili.

B. Idara ya Utawala na fedha (Administration and Finance Department)

Idara ya  utawala na fedha  ina jukumu la kusimamia huduma za Baraza zikiwemo masuala ya uendeshaji wa Baraza, rasilimali watu, rasilimali fedha, mifumo ya uendeshaji na uwekaji kumbukumbu.

Majukumu ya Idara ya Utawala na Fedha.

  • Kutoa huduma za uendeshaji, rasilimali watu na utawala kwa Baraza.
  • Kusimamia masuala ya rasilimai watu kama ajira, mafunzo, upimaji wa utendaji kazi, kupandishwa vyeo, mishahara na stahiki nyenginezo.
  • Kufanya tathmini  ya mahitaji ya wafanyakazi wa ZNBC, kuandaa ripoti ya hali ya utumishi kila baada ya mwaka kwa mujibu wa matakwa ya sheria ya utumishi wa Umma.
  • Kuandaa na kufuatilia mkataba ya utoaji huduma na wateja (Client Service Charter).
  • Kusimamia masuala ya fedha, kutoa huduma za uhasibu,  uwekaji wa kumbukumbu za hesabu, kusimamia mapato na matumizi,  uandaaji wa ripoti za fedha, ulipaji wa mishahara na matayarisho ya mafao ya uzeeni. vi. Kuandaa bajeti na kusimamia utekelezaji wa mpango kazi na mpango wa matumizi wa ZNBC.
  • Kuweka na kuhifadhi kumbukumbu za ZNBC.
  • Kusimamia matumizi na matunzo ya mali za ZNBC ikiwemo vyombo vya usafiri, mitambo, samani, vifaa vya kuandikia na vifaa vya mawasiliano, ix. Kufuatilia, kukusanya na kuratibu mipango ya utumishi na rasilimali watu kwa ZNBC,
  • Kutayarisha ripoti za utekelezaji za majukumu ya ZNBC za miezi mitatu, nusu mwaka na mwaka, xi. Kuandaa mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi wa ZNBC. xii. Kuchapisha nyaraka mbali mbali za ZNBC.
  • Kusimamia masjala ya siri na dhahiri.
  • Kusimamia matengenezo ya ofisi na vifaa na uangalizi wa ofisi.
  • Kutekeleza majukumu mengine yanayoendana na kazi za ZNBC zinazohusiana na uendeshaji, rasilimali watu na fedha.

Vitengo vya Baraza (ZNBC)

Baraza litakuwa na vitengo vitatu vitakavyosimamiwa na Katibu Mtendaji kama muongozo wa Serikali unavyoelekeza. Vitengo hivyo ni kama ifuatavyo:- 

  1. Kitengo  cha elimu, Habari na Mawasiliano
  2. Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani. 
  3. Kitengo cha Manunuzi na Ugavi. 

Kitengo cha Elimu, Habari na Mawasiliano (ICT)

Kitengo hiki kitaongozwa na Afisa Mwandamizi ambaye mamlaka yake ya uteuzi ni Kamati Tendaji ya ZNBC na ataripoti kwa Katibu Mtendaji na atakuwa na sifa za kielimu kuanzia shahada ya kwanza katika fani ya teknologia ya habari, sayansi ya kompyuta na hisabati na fani zinazohusiana na hizo pamoja na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu.

Majukumu ya Kitengo cha Elimu, Habari na Mawasiliano

  • Kubuni na kuanzisha mifumo ya teknologia ya habari na mawasiliano katika ZNBC.
  • Kusimamia mifumo ya masuala ya teknologia ya habari na mawasiliano ya ZNBC.
  • Kuandaa na kuendeleza tovuti na kanzi data za ZNBC (Website & Database).
  • Kutayarisha na kusimamia mfumo wa uwekaji taarifa (MIS).
  • Kushauri uongozi juu ya matumizi bora ya mfumo wa mawasiliano ya habari na vifaa “hardware & software”.
  • Kutunza kumbukumbu za matumizi ya mifumo ya kompyuta.
  • Kutoa ushauri kuhusu upatikanaji wa vifaa vya TEHAMA.
  • Kuratibu na kuziunganisha taasisi nyengine za kitaifa na kimataifa kwa nia ya kukuza mahusiano na ushirikiano.
  • Kusimamia masuala mbalimbali ya kiitifaki ya ndani ya ZNBC.
  • Kuandaa mikutano na waandishi wa habari na wadau wengine.
  • Kuweka taarifa mbali mbali za ZNBC katika tovuti wakati.

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani

Kitengo hiki kitaongozwa na Afisa Mwandamizi ambaye mamlaka yake ya uteuzi ni Kamati Tendaji ya ZNBC na ataripoti kwa Katibu Mtendaji na atakuwa na sifa za kielimu kuanzia shahada ya kwanza katika fani ya usimamizi wa fedha na fani zinazohusiana na hizo pamoja na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu. Kitengo hiki kitaongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani.

Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani

  1. Kufanya ukaguzi wa mapato na matumizi ya fedha kulingana na taratibu za sheria na kutoa taarifa.
  2. Kukagua na kutoa taarifa zinazoendana na mambo ya fedha na uendeshaji kama zilivyoainishwa katika Sheria, Kanuni na taratibu zote za fedha zilizopo ili kufanikisha usimamizi wa matumizi ya rasilimali za ZNBC. iii. Kukagua na kutoa ripoti juu ya mapato na matumizi kulingana na mafungu sahihi ya fedha.
  3. Kukagua na kutoa ripoti juu ya ukaguzi mwengine na uendeshaji zilizotumika katika kuandaa taarifa za mwisho kila mwaka pamoja na taarifa nyingine zote zinazotakiwa kisheria.
  4. Kushauri juu mfumo sahihi wa matumizi na udhibiti wa rasilimali za ZNBC.
  5. Kuandaa ripoti ya utekelezaji na kuiwasilisha kwa Katibu Mtendaji.
  6. Kufanya kazi nyingine zote zinazohusiana na masuala ya ukaguzi na utunzaji wa rasilimali akazopangiwa na uongozi.

Kitengo cha Manunuzi na Ugavi

Kitengo hiki kitaongozwa na Afisa Mwandamizi ambaye ataripoti kwa Katibu Mtendaji na mamlaka yake ya uteuzi ni Kamati Tendaji ya ZNBC na atakuwa na sifa za kielimu kuanzia shahada ya kwanza katika fani ya manunuzi na ugavi na fani zinazohusiana na hizo pamoja na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu. Kitengo hiki kitaongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi.

Majukumu ya Kitengo cha Manunuzi na Ugavi.

i. Kusimamia shughuli zote zinazohusiana na manunuzi na uondoshaji wa vifaa chakavu vya ZNBC.

ii. Kusaidia utekelezaji wa majukumu ya bodi ya zabuni.

iii. Kutekeleza maamuzi ya bodi ya zabuni iv. Kushirikiana na idara ya uhakiki mali na manunuzi kuhusu masuala ya manunuzi

v. Kutoa huduma za sekretarieti ya bodi ya zabuni, kama vile kuitisha vikao, kuandaa kumbukumbu na kutoa ushauri.

vi. Kuandaa mpango wa manunuzi wa ZNBC wa mwaka vii. Kupanga shughuli za manunuzi na uondoshaji wa vifaa chakavu katika ZNBC.

viii. Kupendekeza taratibu za manunuzi na uondoshaji wa vifaa chakavu kwa uongozi. ix. Kuangalia na kuandaa taarifa ya mahitaji ya manunuzi ya vifaa na huduma za ZNBC.

ix. Kutayarisha nyaraka, matangazo, kusimamia zabuni na kuweka taarifa. 

x. Kushiriki katika uandaaji wa mikataba inayohusiana na masuala ya manunuzi na uondoshaji wa vifaa chakavu.

xi. Kutunza kumbukumbu zinazohusiana na manunuzi na uondoshaji wa vifaa chakavu.

xii. Kuratibu shughuli zinazohusiana na manunuzi na uondoshaji wa vifaa chakavu katika Idara zote za ZNBC.

xiii. Kuandaa taarifa za zabuni za ZNBC.

xiv. Kufanya kazi nyingine zote zinazohusiana na majukumu ya kazi akayopangiwa na uongozi.

CHANGAMOTO ZA MUUNDO WA SASA

  1. Ukosefu wa Muundo rasmi wa Baraza la Taifa la Biashara   unapelekea kushindwa kuendana na mabadiliko mbalimbali ya utekelezaji wa majukumu na mahitaji halisi ya ZNBC kulingana na wakati, jambo ambalo litasababisha kutofikiwa kwa malengo yaliyokusudiwa kutokana na mpango kazi ulioainishwa na ZNBC katika kipindi husika.
  2. Kukosekana kwa Muundo wa ZNBC kunapelekea kukosekana kwa mgawanyo wa uwajibikaji wa majukumu (chain of Command) unaosababisha watendaji wote kuripoti kwa Katibu Mtendaji moja kwa moja. Hali hii inasababishwa kuwa na urasimu wa kiutendaji kwa kuwa Mtendaji Mkuu kwa kuwa na Majukumu mengi yanayosababishwa na kutokuwapo kwa Wasaidizi wenye Dhamana za Kimuundo uliopata ithibati kutoka Serikalini.
  3. Kukosekana kwa Muundo wa Baraza la Taifa la Biashara uliioithinishwa kunapelekea kukosekana kwa maslahi kwa Watendaji wakuu wa Baraza la Taifa la Biashara kulingana na majukumu wanayoyatekeleza ikizingatiwa kwamba watendaji hao ni wasaidizi wakuu wa Katibu Mtendaji.
  4. Kukosekana kitengo cha Tehama ambacho ni muhimu kwani kinahusika na majukumu ya kutoa huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano ndani ya Baraza la Taifa la Biashara.
  5. Kukosekana kwa kitengo cha Uhusiano,  Kitengo  ambacho ni muhimu sana kwani ndio  yenye jukumu la kulisemea ZNBC  kwa kushughulikia masuala ya mahusiano kati ya ZNBC na Taasisi nyengine.

MCHORO WA MUUNDO WA SASA