Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda

BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA ZANZIBAR

Kamati Tendaji ya ZNBC

Kamati Tendaji inaundwa kwa mujibu wa Kifungu namba 14 cha Sheria namba 10 mwaka 2017, Sheria ya kuundwa kwa Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar. Katika utekelezaji wa kazi zake Kamati Tendaji inaongozwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ.

Majukumu ya Kamati Tendaji

Kamati Tendaji itakuwa na majukumu yafuatayo kama ilivyoainishwa katika Kifungu namba 16 cha cha Sheria namba 10 mwaka 2017, Sheria ya Kuundwa kwa Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar.

  • Kuandaa Mikutano ya Baraza.
  • Kaanda ajenda za Mikutano ya Baraza.
  • Kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo na maamuzi ya Baraza.
  • Kusimamia kazi za Katibu Mtendaji wa Baraza kwa ajili ya kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yamefikiwa.
  • Kuanzisha Muundo wa Taasisi kwa ajili ya kuweka utaratibu wa utekelezaji wa kazi za Baraza.